Home news MAANDALIZI MUHIMU KUELEKEA MSIMU MPYA

MAANDALIZI MUHIMU KUELEKEA MSIMU MPYA



 AMINI kwamba kila kitu kinawezekana ikiwa utaamua kukifanya kwa juhudi isiyo ya kawaida bila kukata tamaa huku ukimtanguliza Mungu kila wakati.

Maandalizi ya Ligi Kuu Bara kwa sasa yanakaribia kufika ukingoni kwa kuwa ligi inakwenda kuanza na ipo njiani hilo lipo wazi kwa kila mmoja na watu wote Tanzania wapenda michezo wanalijua hilo.

Jambo la msingi ambalo linapaswa kufanyika kwa sasa ni kuweza kuona hali inakuaje na kila kitu kinawezaje kutimizwa.Ukijiandaa kufeli utakwama mapema lakini ukijiandaa kufaulu inakuwa ni rahisi kufikia malengo hayo.

Hali hii inaleta picha nzuri kule ambako tunatarajia kwenda kutokana na kila mmoja kuwa na kitu ambacho anakifikiria kwa sasa na anakitenda kwa wakati.

Ukweli upo wazi kuwa timu zinapoanza ligi zinakuwa na malengo yao hivyo ni muhimu kila mmoja kuangalia ni namna gani timu inaweza kufanya kazi katika kufikia malengo ambayo amejiwekea.

Hakuna mafanikio ambayo yatapatikana kwa timu ikiwa hakutakuwa na juhudi kuanzia kwa wachezaji katika kufuata kile ambacho wanaelekezwa katika benchi a ufundi.

Kilicho nyuma ya ushindi ndani ya uwanja ni lazima kila mmoja afanye kazi kwa juhudi na inawezekana kwa kuwa kila mmoja anahitaji kushinda.

Imani yangu ni kuona kwamba wakati ujao ambao utakuwa na ushindani mkubwa kila timu itakuwa inajua kwamba inahitaji jambo gani.

Kikubwa kinachohitajika ni maandalizi makini na kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa wakati sahihi itaongeza ushindani na kuleta matokeo mazuri.

Ni bahati mbaya kila wakati timu nyingi kuanza kuonyesha ushindani kwenye mzunguko wa pili ambao ni wa lala salama jambo ambalo linawaongezea ugumu kufanya vizuri.

Zile ambazo zinapanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza zina kazi kubwa ya kuanza kufanya maandalizi ili ziweze kuleta ushindani wa kweli ndani ya ligi.

Kupanda ni rahisi licha ya kwamba huko kuna ushindani lakini ukishuka kurudi ni wimbo mwingine ambao ni mgumu kuimbwa na kupendwa pia na wenye timu Bongo.

Kwa timu ambazo zimepanda bado zinapaswa kukumbuka pongezi ambazo wanapewa kwa wakati huu ni lazima wazilipe kwa kufanya kazi kwa vitendo uwanjani.

SOMA NA HII  UHALISIA WA MANARA NA SOKA LA TANZANIA

Kupitia kwa wale ambao walipanda na kushuka basi kuwape nguvu ya kupambana wale ambao wamepanda na wasisahau kwamba kuna suala la kushuka pia.

Tunataka kuona timu ikipanda kwenye ligi iwe na uwezo na vigezo vya kuhimili mikikimikiki ya huku kwani hakuna kuzubaa ni mwendo wa kukimbizana.

Kila timu ifanye kazi kwa kushirikiana katika kusaka mafanikio na hiyo itaongeza nguvu kwa kila mchezaji kuweza kupata ushindi na kufanya mabo ambayo ni ya tofauti.

Wale ambao wameanza kukata tamaa wakati ligi ikiwa haijaanza basi ni muhimu kwa sasa kila timu kujipanga upya na kufanya kazi kwa juhudi.

Maandalizi mazuri ni siri ya ushindi na kushirikiana katika kila jambo ni muhimu kwa ajili ya wakati huu ndani na nje ya uwanja.

Hakuna ambaye anapenda kuona timu yake inashindwa kupata matokeo chanya ama hakuna ambaye anapenda kuona kwamba timu yake inashuka.

Duniani kote kila timu inahitaji ushindi kwa namna yoyote hata ikiwa ni mechi ya kirafiki jambo ambalo linahitajika ni ushindi.

Ushindi haupatikani kwa wepesi lazima utafutwe kwa ushindi mkubwa ili uweze kupatikana kwa kuwa hata kutumia nguvu kusaka ushindi ni ushindi pia.

Zile timu ambazo zinakazi kimataifa zinapaswa pongezi kwa kuwa kazi hiyo ni kubwa na kila mmoja anafurahi pale timu inapopata matokeo chanya na inapokwama huwa inakuwa ni gazi.