Home Yanga SC KAZE:KUPOTEZA KWETU NI FUNZO, BADO HATUJAKATA TAMAA

KAZE:KUPOTEZA KWETU NI FUNZO, BADO HATUJAKATA TAMAA


 CEDRICK Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kichapo walichokipata mbele ya Coastal Union ni funzo kwao ili kuweza kufanya vizuri kweye mechi zao zijazo na hawana wa kumlaumu ndani ya uwanja .


Machi 4, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kwenye harakati za kusaka pointi tatu baada ya dakika 90 kukamilika ubao ulisoma Coastal Union 2-1 Yanga.

Ushindi huo kwa Coastal Union unawafanya iwe timu ya kwanza kushinda mbele ya Yanga ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 kwa kuwa ilicheza jumla ya mechi 21 bila kuambulia maumivu ya kufungwa.

Kaze amesema kuwa vijana wake walipambana kusaka ushindi ila mambo yalikuwa magumu kwao hivyo hawana wa kumlaumu.

β€œIlikuwa ni kazi kubwa kwa vijana na walipambana kusaka ushindi ila haikuwa na namna kwetu tukapoteza na kwa sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo hakuna wa kumlaumu.

β€œNiseme kwamba kupoteza kwetu ni sehemu ya mchezo na tutajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo mashabiki watupe sapoti bado tupo imara,” amesema.


Leo Machi 7, Polisi Tanzania inawakaribisha Yanga kenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Mzunguko wa kwanza walipokutana uwanjani ubao ulisoma, Yanga 1-0 Polisi Tanzania hivyo leo utakuwa ni mchezo wa kulipana kisasi.

SOMA NA HII  YANGA WAJA NA JIPYA KUHUSU MSIMU WA 2022/23 ISHU IKO HIVI