Home Habari za michezo YANGA WAJA NA JIPYA KUHUSU MSIMU WA 2022/23 ISHU IKO HIVI

YANGA WAJA NA JIPYA KUHUSU MSIMU WA 2022/23 ISHU IKO HIVI

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

KLABU ya Yanga Agosti 7 anatarajiwa kuzindua Documentary ya msimu wa kihistoria 2022/23, Dar es Salaam.

Afisa Habari Yanga Ally Kamwe amesema hayo Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Documentary hii iliyotengenezwa kwa utaalamu mkubwa na yenye hadhi ya kuonyeshwa sinema inakwenda kuwaonyesha wanachama na mashabiki wetu maudhui mengi na makubwa ambayo hauwezi kuyapata sehemu yoyote yaliyoiwezesha Klabu yetu kuwa na msimu wa mafanikio na wa kihistoria”

Kamwe amesema Documentary hiyo ni sehemu ya kwanza kwani Yanga itakuja na mradi mkubwa wa historia ya Klabu toka kuanzishwa kwake, kwa kuandikwa kitabu cha historia ya timu hiyo na kuwashirikisha waandishi nguli nchini.

SOMA NA HII  WAKATI MASHABIKI 'WAKIENJOY'....KUMBE NABI 'KAVURUGWA' NA USAJILI WA MUSONDA YANGA...