Home Habari za michezo MASTAA YANGA WAZIDI KUISHIKA CAF KILA KONA ….SIMBA MHHHH…

MASTAA YANGA WAZIDI KUISHIKA CAF KILA KONA ….SIMBA MHHHH…

Habari za Yanga leo

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limetoa orodha ya wachezaji 11 wanaounda kikosi cha kwanza cha wiki cha CAF baada ya kumalizika kwa mzunguko wa tano wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwenye kikosi hicho, ‘Wananchi’ Yanga wameingiza wachezaji watatu ambao ni beki Kouassi Attoulah Yao, kiungo Stehanie Aziz Ki na mshambuliaji Kennedy Musonda wakati watani zao Simba wakiwa hawajaingiza hata mchezaji mmoja.

Itaku kumbukwa kuwa, katika mchezo uliopigwa wekend iliyopita Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 kutoka kwa CR Belouizdad na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, wakati wenzao Simba wakitoa sare na ASEC Mimosas na kuwafanya wasubiri mpaka mchezo wa mwisho watakaoupiga na Jwaneng Galaxy Jumamosi ijayo.

Licha ya nyota watatu wa Yanga wanaounda kikosi cha CAF cha wiki, nyota wengine ni kipa Mostafa Ahmed Abdelaziz Mohamed Shobeir wa Al Ahly ya Misri, Badr Gaddarine wa Wydad ya Morocco.

Wengine ni Yassine Meriah wa Espérance ya Tunisia, Teboho Mokoena wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Marcelo Allende wa Mamelodi, Glody Likonza wa TP Mazembe ya Congo DR, Houssem Tka na Yan Medeiros Sasse wote wa Espérance.

SOMA NA HII  YANGA NAO WAONJA LADHA YA USHINDI