Home Habari za michezo KUHUSU MO DEWJI KUSHUKURIWA KWA YANGA KUTINGA ROBO CAF…HIVI NDIVYO KAMWE ALIVYOIJIBU...

KUHUSU MO DEWJI KUSHUKURIWA KWA YANGA KUTINGA ROBO CAF…HIVI NDIVYO KAMWE ALIVYOIJIBU HOJA HII..

Habari za Yanga SC

Afisa habari wa Yanga Ali Kamwe amejibu kuhusu Afisa habari wa Simba Ahmed Ally kusema kuwa kufuzu kwa Yanga wa kushukuriwa ni Mo Dewji.

“Limeulizwa swali hapa kwamba mimi kama msemaji wa Klabu ya Yanga ninapaswa kuilinda brand ya Yanga ili watu wasiizungumze tu vibaya na kuichafua klabu, na akasema kuwa, hivi karibuni wameibuka watu wanasema mafanikio ya yanga wapongezwe watu wengine ambao sio Yanga.

“Mimi nikwambie tu kwa kifupi kwamba, wahenga waliwahi kunena wakasema ‘mjinga mpe cheyo, halafu wewe endelea na yako’, sisi wajinga tumewapa cheo, yetu yanakwenda mbele,” amesema Kamwe.

Akizungumza jana na wanahabri, Ahmed Ally alisema; “Kufuzu kwa Yanga SC katika hatua ya robo fainali wa kushukuriwa ni Rais wa heshima wa Simba ni Mohammed Dewji na wa pili ni Simba SC.

“Wakati Mo anakuja kuwekeza Simba alisema vision yake ni kushinda ubingwa wa Afrika na baada ya hapo tukaanza mchakato wa kutawala soka la Afrika.

“Wakati Mohammed Dewji anatengeneza dira ya kutawala soka la Afrika vilabu vingine vilikuwa vimelala usingizi wa pono, vilikuwa haviwazi kushindana Afrika na kusumbua.

“Baada ya miaka mitano ndio na wengine wameamka na wenyewe kutaka kuanza kufanya vizuri. Kama Simba SC na Mohammed Dewji tungeendelea kulala basi hadi sasa hakuna klabu yoyote Tanzania ingekuwa na hasira

“Malengo ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika ndio maana nasema robo fainali yao ya kwanza wa kushukuriwa ni Mohammed Dewji ndio aliwaamsha watu kutoka kwenye usingizi. Huu ndio ukweli ambao utadumu milele.”

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KURUDI BONGO...MBRAZILI SIMBA AKABIDHIWA 'FAILI JEUSI' LA CAF...