Home Habari za michezo BAADA YA KUSIKIA HISTORIA YA JWANENG KWA SIMBA….BENCHIKHA KAGUNA WEEH….KISHA AKASEMA HILI…

BAADA YA KUSIKIA HISTORIA YA JWANENG KWA SIMBA….BENCHIKHA KAGUNA WEEH….KISHA AKASEMA HILI…

Habari za Simba leo

Wakati Simba wakijipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa mwisho hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Kocha Mkuu wa Simba Abdelhak Benchikha amesema kuwa hataki historia mbaya ya Simba dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Akizungumza kuelekea mchezo huo Benchikha anasema;

“Galaxy sio timu rahisi ni kama jeshi lisilotabirika, hakuna aliyedhani kama ingeifunga Wydad Casablanca nchini Morocco kwenye mchezo wa kwanza wa makundi, hata hapa Simba rekodi zinaonyesha wamewahi kushtua kwa kushinda hapa, nadhani mashabiki na hata wao wachezaji wanalijua hili na tayari nimeshakaa kikao na wachezaji na kuwakumbusha,”

“Kwenye soka mambo ya kushtua kama haya huwa yanatokea, sitaki historia hii ijirudie hapa chini yangu, nimezungumza nao tukiwa kule ugenini juzi nadhani kila mtu ataelewa tulizungumza nini. Tunatakiwa kujipanga na vita nzito ya mchezo huu, nawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi kuwapa hamasa wachezaji wao wakiwa vitani ndio kitu pekee tunahitaji kutoka kwao,”

“Ili kushinda tunahitaji kufunga mabao ya kutosha lakini pia kujilinda vizuri lakini kule mbele bado hatujawa imara zaidi tutawaongezea wachezaji mbinu za kutengeneza nafasi na kuzitumia kwenye hizi siku tutakazokuwa kambini.” Kuonyesha msisitizo, kocha huyo hajawapumzisha wachezaji.

SOMA NA HII  WAKATI WAARABU WAKIZIDISHA PRESHA YA KUMTAKA MAYELE...YANGA WAIBUKA NA HILI JIPYA...MWAKALEBELA ASEMA NI NGUMU...