Home Habari za michezo KOCHA MPYA YANGA HUYU HAPA….HIYO CV YAKE TU..MBRAZILI WA SIMBA AKASOME UPYA…

KOCHA MPYA YANGA HUYU HAPA….HIYO CV YAKE TU..MBRAZILI WA SIMBA AKASOME UPYA…

Kocha Mpya wa Yanga

HATIMAYE Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Timu ya Yanga SC imemtambulisha rasmi Kocha Mkuu, Miguel Angel Gamondi kuinoa timu hiyo msimu ujao akichukua nafasi ya Nasreddine Nabi aliyemaliza mkataba wake.

Kocha huyo raia wa Argentina ametambulishwa leo na Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ally Kamwe wakati wa mkutano mkuu unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).

Kocha huyo ana uzoefu mkubwa na soka la Afrika kwani kashawahi kuwa kocha mkuu katika klabu za Mamelodi Sundowns, USM Alger, Wydad Casablanca, Platinum Stars,CR Belouzidad na ASEC Mimosas.

Gamondi pia amewahi kuwa kocha msaidizi timu ya taifa ya Burkina Faso na Esperance Sportive de Tunis.

SOMA NA HII  ZA NDAANI KABISAAA...HIZI HAPA SABABU ZA MOSES PHIRI KUPOTEANA SIMBA...BALEKE AONGEZA KITU..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here