Home Habari za michezo KIPA MPYA SIMBA HUYU HAPA….JAMAA ANADAKA MPAKA ‘MBU’….

KIPA MPYA SIMBA HUYU HAPA….JAMAA ANADAKA MPAKA ‘MBU’….

Tetesi za Usajili Simba

SIMBA imelazimika kurudisha hesabu zake za kusajili kipa mpya wa kigeni baada ya kuthibitika muda ambao kipa wao namba moja Aishi Manula atakaa nje.

Manula hataweza kuichezea Simba kabla ya Novemba mwaka huu kufuatia kuuguza jeraha alilonalo akiwa ametoka kufanyiwa upasuaji Afrika Kusini.

Simba imeona baada ya kuthibitika hilo haraka wanatakiwa kusaka kipa wa maana atakayetangulia kuanza msimu kama kipa wao namba moja.

Mabosi wa Simba wamesharudi sokoni haraka kuendelea na mchakato huo wa kusaka kipa huyo haraka atakayekuja kusaidiana na kipa wao kinda Ally Salim.

Simba haitakuwa na kipa wao namba mbili Benno Kakolanya ambaye tayari alishamaliza na Singida Fountain gate alikosaini mkataba wa miaka miwili kitambo.

Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amewaambia mabosi wa Simba anahitajika haraka kipa mpya kwa kutokana na ripoti ya Manula sambamba na mabeki wawili wa kati, huku majina yanayotajwa ni Fabien Mutombora na Alfred Macumu Mudekereza wanaoidakia kwa sasa Vipers ya Uganda timu aliyowahi kufanya kazi na kocha huyo wa Simba.

Mbali na makipa hao, inaelezwa mabosi wa Simba wana jina lingine la kipa kutoka Zambia ambaye hata hivyo hajatajwa wala kufahamika timu anayoichezea kwa sasa.

Simba pia inataka mabeki wawili wa kuchukua nafasi ya Joash Onyango na Mohamed Outtara ambaye tayari ameshapewa ‘thank you’ yake ndani ya klabu hiyo.

SOMA NA HII  KAMWAGA: SIMBA NA PABLO FRANCO; HATUA MOJA TU LAKINI HATUA KUBWA SANA...