Home Habari za michezo KUELEKEA KOMBE LA DUNIA QATAR…ITV NA BBC ZAPIGANA VIKUMBO KUITAKA SAINI YA...

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA QATAR…ITV NA BBC ZAPIGANA VIKUMBO KUITAKA SAINI YA ‘KIBONGE’ WAYNE ROONEY…


Huenda mkongwe wa soka kutokea England, Wayne Rooney akalazimika kukaa mbali na familia yake kwa kipindi kirefu zaidi baada ya tetesi kuwa yuko kwenye mazungumzo ya kazi nyingine ya mwishoni mwa mwaka.

Kwa mujibu wa Sunsport kampuni za ITV na BBC zimo katikati ya mchuano mkali wa kumpatia mshambuliaji huyo mkataba wa kuwa mtoa maoni/mchambuzi wa timu ya taifa ya England kwenye mashindano ya kombe la dunia 2022 nchini Qatar.

Hivi sasa Rooney amehamia Marekani ambako anaiongoza DC United na msimu wao wa sasa utafikia mwisho mnamo mwezi Oktoba hivyo kumpa muda mzuri kuweza kwenda Qatar kufanya kazi.

SOMA NA HII  KAMA UTANI VILE KOCHA NAMUNGO ABWAGA MANYANGA