Home Uncategorized SIMBA SC YATIKISA HOTUBA YA WAZIRI MKUU BUNGENI

SIMBA SC YATIKISA HOTUBA YA WAZIRI MKUU BUNGENI

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara,Simba Sc jioni hii wametikisa na kuibua shangwe Bungeni wakati Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akifunga hotuba yake ya kuhitimisha Bunge la Bajeti.

Majaliwa aliibua shangwe hizo na Bunge kurindima kwa shangwe baada ya kuzungumzia ubora wa Simba ya msimu huu pamoja na mafanikio yao ya hivi karibuni kwenye ligi na mashindano ya kimataifa huku akihoji kwa mafanikio ya Simba nini faida ya mkuki?.

Alisifia hatua ya Simba kuvuka kwenye mechi ngumu na kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku akishangilia na wabunge wengi akiwemo spika Job Ndugai ambaye alikuwa akichombeza maneno ya hapa na pale kusherehesha hotuba hiyo.

Alizidisha shangwe za wabunge baada ya kutangaza kwamba Simba inakaribia kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu Bara ikiwa imesaliwa na mechi tisa, huku akiwakejeli Yanga kwamba kama Simba inaweza kutangaza ubingwa ikiwa na mechi kibao mkononi;

“Nini faida ya mikuki? Kama klabu inaweza kutangaza ubingwa kabla haijamaliza michezo yote nini faida ya mkuki?,” alisema huku akizidi kushangiliwa.

Waziri Mkuu alisema kuwa Simba imefanya mengi katika miaka ya hivi karibuni na inastahili sifa.

“Ili kuonyesha ubora wa timu hiyo mfungaji anayeongoza kwa kufunga mabao ni Meddie Kagere ambaye amefunga magoli 19,”alisema na kukoleza kwamba “Hatujaona timu ya Wananchi ikiongoza kwenye magoli.”

“Mheshimiwa Spika hatua hii haiwezi kufikiwa na timu yoyote kwa vile mikuki mingi ni butu, mkuki wenye ncha kali upo Simba SC,” alisema Waziri Majaliwa.

Katika horuba yake Majaliwa alimpongeza Mbwana Samatta wa Astonvilla ya England, Simon Msuva wa Difaa ya Moroco, pamoja na wachezaji wengine na timu mbalimbali za Taifa na wasanii waliofanya vizuri katika kipindi cha hivikaribuni.

SOMA NA HII  MBELGIJI SIMBA ATOA SABABU ZA TIMU YAKE KUBORONGA KIWANGO