Home Uncategorized BENO KAKOLANYA MLINDA MLANGO NAMBA MBILI WA SIMBA ATUMIA DAKIKA 720 KUTWAA...

BENO KAKOLANYA MLINDA MLANGO NAMBA MBILI WA SIMBA ATUMIA DAKIKA 720 KUTWAA TAJI, ATUNGULIWA MABAO SITA


BENO Kakolanya mlinda mlango namba mbili wa Simba amefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20 ndani ya Simba akiwa amekaa langoni kwenye jumla ya mechi 8 kati ya 34 ambazo Simba imecheza. 

Kakolanya aliibukia Simba kwa dili la miaka miwili akitokea Klabu ya Yanga ambapo huko alikuwa ni kipa namba moja.

Kwenye mchezo wa kukabidhiwa taji uliochezwa Uwanja wa Majaliwa yeye alikaa langoni na kutimiza mchezo wake wa nane na dakika 90 zilikamilika kwa Simba kutoshana nguvu bila kufungana na Namungo huku Kakolanya akiweka lango salama.

Kiungo wao mchezeshaji ambaye gari limewaka kwa sasa Clatous Chama mwenye pasi nane za mabao akiwa ametupia pia mabao mawili kati ya 69 hakuweza kucheza mchezo huo. 

Kakolanya ametumia jumla ya dakika 720 uwanjani huku akitoka na clean sheet tatu na amefungwa jumla ya mabao sita kati ya mabao 16 ambayo Simba imefungwa.

Hilo linakuwa taji la 21 kwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck pamoja na Seleman Matola ambaye ni msaidizi wake.

Julia 12 wana kazi ya kukutana na Yanga kwenye mchezo wa nusu fainali Kombe la Shirikisho ambao wapo Kwenye ubora wao kwani mchezo wao uliopita waliinyoosha Kagera Sugar kwa ushindi wa bao 1-0 Mchezo wa Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  SAMATTA ATOA OFA KWA WACHEZAJI WOTE STARS