Home Uncategorized MANCHESTER UNITED SIO WATU WAZURI WAISHUSHIA MVUA YA MABAO ASTON VILLA YA...

MANCHESTER UNITED SIO WATU WAZURI WAISHUSHIA MVUA YA MABAO ASTON VILLA YA MBWANA SAMATTA


PAUL Pogba, nyota wa Manchester United alikomelea msumari wa mwisho kwa Aston Villa kwenye mchezo wa Ligi Kuu England wakati wakiibamiza kwa mabao 3-0.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Villa Park umewaachia majonzi mazito vijana wa Villa ambapo nyota wa Tanzania Mbwana Samatta anakipiga kwa sasa.

Hicho kinakuwa ni kichapo cha pili mfululizo kwa Aston Villa kutoka kwa timu kubwa kwani mchezo wake uliopita wakati Samatta akitumia dakika 17 mbele ya Liverpool Uwanja wa Anfield waliambulia kichapo cha mabao 2-0.

Mvua ya mabao kwa Aston Villa kutoka kwa Manchester United ambao wamewaka baada ya mapumziko yaliyosababishwa na Virusi vya Corona ilianza dakika ya 27 kupitia kwa Bruno Fernandes dakika ya 27 akifunga kwa mkwaju wa penalti.

Greenwood kinda ambaye Manchester United wamemchagua kuwa mchezaji bora wa mchezo yeye alipachika bao dakika ya 45 na mwisho wa yote Pogba alikamilisha msumari wa mwisho dakika ya 58 na kuifanya Manchester United kusepa na pointi tatu mazima.

Ushindi huo unaifanya Manchester United kufikisha jumla ya pointi 58 ikiwa nafasi ya tano huku Aston Villa ikibaki na pointi zake 27 ambazo zinazidi kudidimiza matumaini ya timu hiyo kubaki ndani ya Ligi Kuu England msimu ujao.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA MTIBWA SUGAR