Home Habari za michezo SHABIKI BILIONEA WA MAN UTD ASHINDWA KUVUMILIA VIPIGO…AAMUA KUWEKA MZIGO KUINUNUA KLABU...

SHABIKI BILIONEA WA MAN UTD ASHINDWA KUVUMILIA VIPIGO…AAMUA KUWEKA MZIGO KUINUNUA KLABU HIYO…


Bilionea Sir Jim Ratcliffe, ambaye anamiliki timu ya waendesha Baiskeli Ineos Grenadiers, yuko tayari kuinunua Manchester United na wachezaji wa zamani watahusishwa pamoja na Meneja Mkuu wa Grenadiers Sir Dave Brailsford.

Bilionea huyo wa Uingereza, ambaye ana utajiri wa dola Bilioni 7.18, kulingana na Bloomberg, hakufanikiwa katika ombi lake la dakika za mwisho la Euro Bilioni 4.25 kuinunua Chelsea mwezi Mei mwaka huu, huku mfanyabiashara Mmarekani Todd Boehly akifanikiwa kuipata klabu hiyo, na Ratcliffe sasa ameelekeza mawazo yake kwa Mashetani Wekundu.

Nia yake inakuja baada ya ripoti ya Bloomberg kusema kwamba familia ya Glazer ambao wamemiliki United tangu 2005, wanafikiria kuuza hisa chache katika klabu hiyo.

Majadiliano ya awali yamefanyika kuhusu kuleta mwekezaji mpya, kulingana na taarifa kutoka Shirika la Utangazaji la Sky Sports, ambalo linamtaja Bilionea Ratcliffe kama mtu tajiri wa sita nchini Uingereza.

Msemaji wa Ineos alisema kampuni hiyo ingependelea kununua hisa ndogo kwa nia ya kuja kuinunua klabu hiyo kabisa.

SOMA NA HII  TETESI : KOCHA WA AL AHLY KUTUA SIMBA SC...MPANGO MZIMA UKO NAMNA HII...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here