Home Habari za michezo USHINDI WA GOLI 3-0 DHIDI YA GEITA WAMRUDISHA MJINI AHMED ALLY…AANZA TAMBO...

USHINDI WA GOLI 3-0 DHIDI YA GEITA WAMRUDISHA MJINI AHMED ALLY…AANZA TAMBO NA MADONGO KWA YANGA TENA…


Ushindi wa 3-0 dhidi ya Geita Gold FC umeifanya Klabu ya Simba SC kutangaza mpango na mkakati wa msimu huu wa 2022/23 ambao ulianza rasmi juzi Jumanne (Agosti 15).

Akizungumza na Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu hiyo yenye Maskani yake Msimbazi-Dar es salaam Ahmed Ally amesema, msimu huu wamekuja na mbinu za kukusanya alama tatu katika michezo yote ya mzunguuko wa kwanza.

Ahmed amesema hawataki kurudi makosa waliyoyafanya msimu uliopita ya kuacha alama nyingi katika mzunguuko wa kwanza, hali ambayo iliwafanya wateseke mzunguuko wa pili na kujikuta wakipoteza Ubingwa mikononi mwa watani zao Young Africans.

“Msimu huu tumepanga kuja na mbinu mpya za kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu, tulichokipanga ni kuchukua alama tatu za kila mchezo tutakaocheza katika mzunguuko huu wa kwanza.

“Tunataka kukusanya alama nyingi mapema katika mzunguuko huu kabla ya kuingia mzunguuko wa pili ambao kila msimu huwa unakuwa mgumu zaidi kutokana na timu kukamiana.”

“Msimu uliopita tulianza kwa Presha ya chini ambayo ilitusababishia kupata alama hafifu, hivyo hatutaki kurudia kosa msimu huu, kwa sababu tumedhamiria kurejesha heshima yetu ya kuwa mabingwa.” amesema Ahmed Ally

Ikumbukwe kuwa msimu uliopita, Simba SC ilikusanya alama 31 kati ya 45 baada ya kumaliza mzunguuko wa kwanza, ikicheza michezo 15 ikishinda tisa, sare nne na kupoteza mbili.

SOMA NA HII  HII HAPA NJIA YA MAYELE KUIBUKA MFUNGAJI BORA AFRIKA...MECHI MBILI TU ANABEBA KIATU CHA DHAHABU....