Home Uncategorized SINGIDA UNITED YACHAPWA TENA, MAMBO BADO MAGUMU

SINGIDA UNITED YACHAPWA TENA, MAMBO BADO MAGUMU



SINGIDA United iliyo chini ya Ramadhan Nswazurimo imeendelea kupoteza mechi zake za Ligi Kuu Bara ambapo jana Machi 4, ilichapwa bao 1-0 na Coastal Union.


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Namfua ulikuwa ni mchezo wa 26 kwa Singida ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kwenye mechi hizo ni mechi mbili tu imeshinda msimu huu ndani ya ligi huku ikipoteza mechi 18 na ina sare sita.

Singida United ipo nafasi ya 20 ikiwa imejikusanyia pointi zake 12.

Mchezo wake uliopita Singida United ilichapwa bao 1-0 na Polisi Tanzania.
SOMA NA HII  KOCHA MANCHESTER UNITED: FERNANDES BADO HAJAFIKIA KUWA RONALDO