Home Uncategorized KAGERA SUGAR: HATUJAKATA TAMAA KUPOTEZA MBELE YA MBEYA CITY

KAGERA SUGAR: HATUJAKATA TAMAA KUPOTEZA MBELE YA MBEYA CITY


UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa kushindwa kufurukuta mbele ya Mbeya City ni sehemu ya mchezo watajipanga kwa ajili ya mechi zinazofuata.

Kagera Sugar, jana ilikubali kichapo cha mabao 3-2 mbele ya Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Kaitaba mabao yote mawili waliyofunga Kagera Sugar yalifungwa na Yusuph Mhilu kwa mkwaju wa penalti.

Kocha Mkuu, Mecky Maxime amesema: “Matokeo tumeyapokea na tunayafanyia kazi makosa yetu ili kuendelea kuwa bora kwani ligi inaendelea na kila timu inatafuta ushindi,”.

Kagera Sugar ipo nafasi ya 7 ikiwa imecheza mechi 26 na ina pointi 38 kibindoni,

SOMA NA HII  HUYU HAPA AMESHIKILIA HATMA YA MSUDAN WA SIMBA