Home Yanga SC MTAMBO WA MABAO YANGA RUKSA KUWAVAA BIASHARA UNITED

MTAMBO WA MABAO YANGA RUKSA KUWAVAA BIASHARA UNITED

 


KIUNGO wa Yanga, Carlos Carlinhos,  mwenye mabao matatu na pasi mbili za mabao amemaliza kuitumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya timu ya Ken Gold.


Carlinhos Alionyeshwa kadi hiyo Februari 27, Uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 baada ya kuonekana akimpiga ngumi beki wa Ken Gold, Boniphace Mwanjonde.

Kutokana na kadi hiyo alikosekana kwenye mechi tatu za ligi kuu ambazo ni  dhidi ya Coastal Union 2-1 Yanga , Uwanja wa Mkwakwani, Polisi Tanzania 1-1 Yanga, na Yanga 1-1 KMC, Uwanja wa Mkapa.

Kumaliza kwake adhabu hiyo, itakuwa ni jukumu la Kaimu Kocha wa Yanga, Juma Mwambusi kumpanga kwenye mchezo ujao  unaotarajiwa kuchezwa Aprili 17, ambao utakuwa ni wa ligi kati ya Yanga dhidi ya Biashara United, Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

Kwenye msimamo Yanga iponafasi ya kwanza ina pointi 51 baada ya kucheza jumla ya mechi 24.

SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KUMUONGEZEA MKATABA ZAWADI MAUYA...BUMBULI ASHINDWA KUJIZUIA...AIBUKA NA HILI JIPYA...