Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUMUONGEZEA MKATABA ZAWADI MAUYA…BUMBULI ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA HILI JIPYA…

BAADA YA YANGA KUMUONGEZEA MKATABA ZAWADI MAUYA…BUMBULI ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA HILI JIPYA…


BAADA ya kumwongeza mkataba wa miaka miwili kiungo mkabaji wake, Zawadi Mauya, Yanga imesema itaendelea na mchakato huo hadi pale watakapomaliza wachezaji wote ambao wanawahitaji kubaki kwa ajili ya msimu ujao.

Juzi jioni Yanga ilitangaza rasmi imempa mkataba mpya kiungo huyo aliyesajiliwa akitokea Kagera Sugar baada ya mkataba wake wa awali kuelekea ukingoni.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema wataendelea kuwasajili na kuwatambulisha mmoja mmoja hadi pale watakapomaliza wachezaji wote ambao wamependekezwa kubaki na benchi la ufundi.

“Tunaendelea mmoja baada ya mwingine, wataendelea kutangaza, nyinyi tulieni tu. Wale ambao bado sisi tunawahitaji hawatoondoka,” alitamba Bumbuli.

Kwa siku chache zilizopita, Yanga imekuwa ikiwaongeza mikataba wachezaji wake muhimu ndani ya kikosi hicho.

“Najisikia furaha nimebaki Yanga kuitumikia timu yangu, nashukuru kwa wananchi kuendelea kuniamini, nyinyi mmetaka kama wanachama na mashabiki, mimi nani nisiweze kukubali kuendelea. Ahsanteni wananchi na wanachama, mimi Zawadi Mauya, bado nipo nipo sana,” alisema mchezaji huyo baada ya kukamilisha usajili wake.

Nyota wengine ambayo Yanga imewapa mikataba mipya ni pamoja na Bakari Mwamnyeto na Kibwana Shomari.

SOMA NA HII  MGUNDA: SIMBA SC HATAYUMBA KISA PHIRI HAYUPO...TUNAVIFAA VYA MAANA...