Home Habari za michezo PEREZ AMKATIA TAMAA MBAPPE…KIINYOONGEE ‘AWACHANA UKWELI’ MASTAA WAKE MADRID..

PEREZ AMKATIA TAMAA MBAPPE…KIINYOONGEE ‘AWACHANA UKWELI’ MASTAA WAKE MADRID..


Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amewambia wachezaji wake na benchi la ufundi kuwa mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe hatojiunga na timu hiyo.

Mabingwa hao wa LaLiga wameshindwa kunasa saini Mbappe dakika za mwisho baada ya kutakiwa kutoa paundi milioni 154 ili kupata huduma ya ‘top scorer’ huyo wa Ligue 1.

Mama mzazi wa Mbappe, Fayza Lamari siku ya Ijumaa amesema kuwa kijana wake ameshafanya hitimisho ya mazungumzo kwa klabu zote mbili.

Baada ya mchezo dhidi ya Real Betis, Perez alikitaarifu kikosi cha Carlo Ancelotti kuwa Mbappe hatojumuika nao kwa mujibu wa vyanzo kutoka ndani ya timu hiyo.

Inadaiwa Madrid ilikuwa tayari kutoa paundi milioni 126.7 ikiwa ni pamoja na mshahara na bonasi.

SOMA NA HII  RASMI...AZAM FC WAZIDI KUTIA MACHUNGU SIMBA SC...WAMALIZANA NA SOPU KWA DAU NONO...ALAMBISHWA MIAKA MITATU...