Home Habari za michezo KUHUSU MBRAZILI KURUDI SIMBA LEO…UKWELI UKO HIVI…KAVUNJA UKIMYA AKIWA HUKO HUKO KWAO...

KUHUSU MBRAZILI KURUDI SIMBA LEO…UKWELI UKO HIVI…KAVUNJA UKIMYA AKIWA HUKO HUKO KWAO BRAZILI…

Habari za Simba leo

KOCHA wa Simba, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho anatua Dar es Salaam leo usiku na kesho atakuwa mazoezini asubuhi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Big Stars Ijumaa.

Kocha huyo inaelezwa pia alihudhuria kozi fupi Ukocha kuongeza ujuzi nchini Brazili ingawa hajafafanua ilikuwa na levo gani.

Robertinho aliondoka nchini kwenda Brazil muda mfupi baada ya kukiongoza kikosi ushinda bao 1-0, dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma, amekosekana kwenye mchezo mmoja wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) timu yake ikipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union na kutinga hatua ya 16 bora.

Akizungumza  muda mfupi kabla hajaondoka nchini alisema sababu iliyomfanya kuondoka ni hati yake ya kusafiria kumalizika muda wa matumizi na hakuwa hata na karatasi moja.

Robertinho alisema kuwa anatarajia kurudi leo saa 4:00 usiku tayari kwa ajili ya kujumuika na timu kuendelea na maandalizi ya mchezo ulio mbele yao ambao ni karata muhimu kwa Simba.

“Kesho (leo) usiku nitakuwa kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam tayari kwa ajili ya kuungana na timu kuendelea na maandalizi ya mchezo ulio mbele yetu,” alisema Kocha huyo mwenye uzoefu na soka la Afrika. “Nimekamilisha mipango iliyonileta huku sasa ni muda wangu wa kurudi na kuendelea pale timu ilipoishia ili kuweza kufikia malengo tuliyokusudia kuyafanya ndani ya timu.”

Simba baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Big Stars (SBS) itacheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Al Hilal kabla ya kusafiri kwenda Guinea tayari kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi itakakokabiliana na wababe Horoya.

Kwa sasa Wekundu hao wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 50.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA COSTAL....YANGA YA GSM WAPANGA KUUWASHA MOTO..YAZANZIBAR BADO YAPO...