Home Habari za michezo FENERBANCE WAAMUA LIWALO NA LIWE KWA SAMATTA…AL AHLY WAMMEZEA MATE KINOMA…

FENERBANCE WAAMUA LIWALO NA LIWE KWA SAMATTA…AL AHLY WAMMEZEA MATE KINOMA…

Mbwana Samatta

WAKATI ikiripotiwa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kuwekwa sokoni na Fenerbahce, miamba ya soka la Afrika, Al Ahly imeamua kujitosa kwa mshambuliaji huyo anayeichezea KRC Genk kwa mkopo baada ya kukwama kwa mchezaji wa kimataifa wa DR Congo Jackson Muleka.

Kwa mujibu wa ripoti ya Sporx, Fenerbahce wanataka kumpiga bei Samatta katika dirisha hili la usajili kwa kuwa yuko nje ya mipango ya kocha wao, Jorge Jesus.

Imeripotiwa, Al Ahly imeelekeza nguvu zao kwa Samatta kutokana na mpango wao wa awali wa kumsajili Muleka kukwama kutokana na Besiktas anayoichezea kutaka kiwango kikubwa zaidi cha fedha.

Inaelezwa Al Ahly inataka kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kati kabla ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA mwezi ujao.

SOMA NA HII  RASMI...MBEYA KWANZA YAWA YA KWANZA KUSHUKA LIGI KUU MSIMU HUU...GEITA GOLD WAISOGELEA CAF KININJA...