Home Habari za michezo KUHUSU FEI TOTO KUIGOME YANGA….INJINIA HERSI AMALIZA ‘JAMBO KIUME’…ISHU NZIMA IKO HIVI..

KUHUSU FEI TOTO KUIGOME YANGA….INJINIA HERSI AMALIZA ‘JAMBO KIUME’…ISHU NZIMA IKO HIVI..

Habari za Yanga

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amefanya kikao na viongozi wa matawi ya klabu hiyo Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali.

Katika mkutano huo uliofanyika juzi Jumamosi, Januari 28, 2023, katika makao makuu ya Klabu, Hersi amewapongeza wanachama wa Yanga kwa kujenga timu imara lakini ametahadharisha sana kuwa maadui wa yanga ni wengi hata wengine sio wa nje bali wako humu humu ndani hivyo ni jukumu la wanachama wa yanga kuipambania timu popote walipo.

Hersi amesisitiza kuwa mafanikio ya kushinda mataji msimu huu yako mikononi mwetu.

Raisi Hersi amewaomba wanayanga kuisapoiti Singida Big stars ili iweze kushinda mechi dhidi ya simba mnamo tarehe 03/02/23 kwani singida ni ndugu zetu wa karibu.

2. SUALA LA METACHA KUSAJILIWA TENA YANGA KWA MKOPO

Hersi ameeleza kuwa golikipa wetu wa pili (Mshery) baada ya kupona jeraha aliumia tena mnamo tarehe 15/01/23 na kupata jeraha litakalomweka nje kwa miezi mingine miwili na aliumia siku ya mwisho ya dirisha dogo la usajili, jambo lililolazimu uongozi kutafuta kwa haraka kipa wa kuziba nafasi ya Mshery.

Uongozi ulifikia mpaka hatua ya kuwaza kumrejesha Dida ili kuwahi muda wa dirisha la usajili kufungwa ndipo baadae Raisi Hersi alipata wazo la kumpigia mmiliki wa SBS na kumuomba Metacha kwa mkopo wa miezi sita, na baada ya kumsajili uongozi umezungumza nae na kumueleza matatizo yake na nini wanatarajia kutoka kwake.

3.KUHUSU FEISAL Hersi amesema Feisal ni mchezaji halali wa yanga na amekuwa akilipwa stahiki zake zote na hata wakati anaongezewa mkataba kiasi cha pesa walichokubaliana na uongozi alilipwa chote taslim jambo ambalo sio la kawaida. Lakini uongozi ulikubali kumpatia kiasi hicho baada ya kuombwa na Familia yake wanahitaji ili wafanyie mahitaji yao.

Hersi ameeleza kuwa wamekuwa wakipanga vikao na mazungumzo ili wamsikilize lakini amekuwa akikwepa kila mara, ameeleza kuwa wale wanaoshauri yanga imwachie hatawasikiliza na kamwe hatafanya hivyo.

4.USHIRIKI CAF Hersi amesema uongozi uko makini na mashindano ya shirisho na amesema ili kuindaa timu vyema wanakusudia timu ikaweke kambi Dubai mapema na kuwa timu itaondoka Januari 7, 23 mara baada ya mechi ya ligi dhidi ya Namungo tarehe.

Pia, amesema uongozi umetengeza jezi za mashindano ya CAF rangi zote kijani, njano na nyeusi zenye nembo za mdhamini mpya wa CAF na zitaanza kuuzwa Jumanne kwenye maduka ya GSM na makao makuu ya klabu baada ya kuzinduliwa Jumatatu.

Na mwisho ameomba tuwahamasishe wanayanga kujisajili kigitali maana usajili kwa sasa unasuasua sana.

SOMA NA HII  KOCHA MAARUFU AFRIKA AIPELEKA YANGA SC NUSU FAINAL CAF...AWAPA MBINU ZA KUPITA...

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here