Home Habari za michezo HII HAPA RATIBA YA MPAPATUKO WA NBC PREMIER LEAGUE LEO…HUKU MAYELE KULE...

HII HAPA RATIBA YA MPAPATUKO WA NBC PREMIER LEAGUE LEO…HUKU MAYELE KULE MPOLE..NANI KUTUNISHA KIBUNDA..?


Leo Juni 25 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo ratiba yake ni moto kwa timu zinazopambana kushuka daraja kwa kuwa hatma yao itaanza kufahamika leo.

Ni Yanga ambao ni mabingwa wa ligi wao hawana presha zaidi ya kuendelea kusaka rekodi za kutofungwa kwa msimu wa 2021/22 ndani ya ligi

Muziki kamili leo utakuwa namna hii:

  1. -Coastal Union v Kagera Sugar ngoma inapigwa saa 8:00 mchana.
  2. Polisi Tanzania v Geita Gold hapa itapigwa saa 8:00 mchana.
  3. Mbeya City v Yanga itapigwa saa 9:30 alasiri.
  4. Biashara United v KMC ngoma itakuwa ni saa 10:00 jioni.

Mbeya Kwanza v Ruvu Shooting hizi zote zipo kwenye hatari ya kushuka daraja kwa kuwa Mbeya Kwanza ipo nafasi ya 16 na pointi 24 huku Ruvu Shooting ikiwa nafasi ya 13 na pointi 26 ngoma itapigwa saa 10:00 jioni.

Dodoma Jiji v Azam FC itapigwa saa 1:00 usiku.

Baada ya mechi za leo timu nyingi zitakuwa zimebakisha mchezo mmoja kukamilisha mzunguko wa pili msimu wa 2021/22.

SOMA NA HII  SIKU KADHAA TOKA ASAJILIWE NA MASHABIKI KUANZA KUMKATAA..KIGOGO SIMBA AIBUKA NA HILI KUHUSU KYOMBO...