Home Habari za michezo SIMBA WAFUNGUKA HAYA BAADA YA KIPIGO 5G

SIMBA WAFUNGUKA HAYA BAADA YA KIPIGO 5G

Habari za Simba

Ngoma imekamilika kwa Simba kupoteza mchezo wa Kariakoo Dabi ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga.

Mabao ya Aziz KI, Max Nzengeli ambaye alifunga mawili, Pacome kwa mkwaju wa penalti na Musonda Kennedy aliyefungulia pazia la mabao dakika ya tatu yametosha kuwatuliza Simba.

Bao pekee la Simba lilifungwa na Kibu Dennis ambaye alitumia pasi ya Saido Ntibanzokiza.Baada ya Simba kunyooshwa mabao hayo matano na watani wa jadi.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram:

”Tumezidiwa na mpinzani wetu na hatimae tumeadhibiwa, hakuna unachoweza kusema zaidi kukiri udhaifu kwa upande wetu. Hili limepita japo linaumiza na haliwezi kufutika katika mioyo yetu lakini muhimu ni kuganga yajayo.

“Tusipoteze focus, mbele yetu tuna mechi nyingi za kupigania malengo yetu Tumepoteza mechi moja bado tuna mechi nyingine mbele za kupigania malengo yetu.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF....KIKOSI CHA WASAUZI CHAANZA KUPUKUTIKA...BEKI WAO WA 'KAZI CHAFU' AUMIA...