Home Habari za michezo MVURUGANO ULIANZIA HAPA KIBU ATAJWA

MVURUGANO ULIANZIA HAPA KIBU ATAJWA

Habari za Simba

Mchambuzi wa soka nchini Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’, amesema Simba ilianza kuharibika baada ya Kibu Denis kuumia.

Mkazuzu ametoa mtazamo wake huo alipokuwa akiuchambua mchezo wa dabi uliomalizika kwa Yanga kuwakanda Simba 5-1 jana Novemba 5, 2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

“Binafsi naona mambo yalianza kuharibika kwa Simba baada ya Kibu kuumia na kulazimika kutoka, mpira ulipoanza tu Yanga walipata goli lililoanzia upande wa kushoto wa Simba baada ya Yanga kufanya shambulizi ambalo liliokolewa lakini kwa haraka Yanga wakatengeneza shambulizi jingine wakafunga.

“Baada ya goli lile la Yanga, Kibu Denis alihamia upande wa kushoto wa Simba kusaidiana na Mohamed Hussein, baada ya hapo Yao akawa hapandi tena mara kwa mara kwenda hadi mwisho wa uwanja kwenye eneo la Simba.

“Ukiangalia magoli mengine manne ya Yanga ambayo yakianza kupatikana kuanzia dakika ya 64, magoli matatu yametokea upande wa kushoto wa Simba ambako Kibu alikuwa anasaidia sana kukaba kabla hajatoka.”

SOMA NA HII  SIMBA YATEMBEZA 4G MBELE YA AL HILAL,MORRISON ATUPIA