Home Habari za michezo KILICHOWATOA MASTAA HAWA YANGA

KILICHOWATOA MASTAA HAWA YANGA

Habari za Yanga leo

Beki wa kulia wa Klabu ya Yanga, Kouassi Attohoula Yao raia wa Ivory Coast, amerejea mazoezini na yupo fiti kwa ajili ya mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate.

Yao alikosekana katika mchezo uliopita dhidi ya Azam baada ya kupata jeraha la enka siku mbili kabla ya mchezo huo ambao tulishinda magoli 3-2.

Daktari wa Yanga SC, Moses Etutu, amesema: “Yao kwa sasa yuko fiti kuivaa Singida. Alipata jeraha la enka siku mbili kabla ya mchezo wa Azam, lakini sasa hivi amerejea vyema mazoezini na yuko tayari kwa mechi.”

SOMA NA HII  DANI ALVES ATIMKA MAZIMA PSG