Home Uncategorized BALAA LA KAKOLANYA LIPO NAMNA HII UWANJANI

BALAA LA KAKOLANYA LIPO NAMNA HII UWANJANI

SIMBA ikiwa imecheza mechi 28 kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara mlinda mlango wake namba mbili Beno Kakolanya amedaka mechi saba.

Kwenye mechi hizo saba sawa na dakika 630 ameruhusu mabao sita ambapo Simba imefungwa jumla mabao 15 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Mechi moja pekee Kakolanya alipoteza pointi tatu huku mechi sita akiongoza kikosi chake kusepa na pointi tatu jumlajumla.

Mechi zake zipo namna hii:-Septemba 25,Simba 4-0 Lipuli, Januari 16, Mbao 1-2 Simba, Januari 19,Alliance 1-4 Simba, Januari 29,Simba 3-2 Namungo,Februari Mosi, Simba 2-0 Coastal Union,Simba 2-1 Polisi Tanzania, Februari 4. Februari 7,JKT Tanzania 1-0 Simba.

SOMA NA HII  KAZE APATA HOFU KUIKABILI NAMUNGO KWA MKAPA