Home Habari za michezo MASHABIKI SIMBA WAPIGWA NA KITU KIZITO SIMBA DAY

MASHABIKI SIMBA WAPIGWA NA KITU KIZITO SIMBA DAY

Wakati kilele cha tamasha la Simba Day kikihitimishwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa , mashabiki mbalimbali wameonekana kulizwa kutokana na kuuziwa tiketi feki.

Mmoja wa shakibi wa timu hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Sudi amesema awali hakuwa na tiketi hivyo alikuja kwa ajili ya kukata uwanjani jambo ambalo limekuwa ni tofauti na matarajio yake.

“Mimi sio mtu wa mitandaoni sana hivyo sikujua kama zimeisha kabla ya tamasha lenyewe kwa sababu nimekuwa na utaratibu wa kukatia tiketi uwanjani,” amesema na kuongeza:

“Kuna mtu hapa uwanjani kaniuzia tiketi ya Sh20,000 ila baada ya kwenda getini ili niingie nikaambiwa ni batili kitu ambacho kimeniuma sana.”

Aidha kwa upande wa shabiki mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mariamu Mbwana amesema aliuziwa tiketi ya Sh10,000 akiamini lengo lake la kuingia uwanjani limefanikiwa ila imekuwa ni tofauti.

“Kupitia hili tamasha nimejifuza kukata tiketi mapema ili kuepuka kadhia hii ya kunipa hasara lakini pia na kukosa nafasi ya kuiona timu yangu,”

Klabu ya Simba ilitangaza kuisha kwa tiketi zote la tamasha hili ikiwa imebaki siku tatu tu kabla ya kufikia kilele chake kilichohitimishwa jana.

SOMA NA HII  SALIM ALLY AISHIKA PABAYA SIMBA..... ISHU IKO HIVI