Home Habari za michezo ONANA AWAPAGAWISHA MASHABIKI MAPEMA SANA, NGOMA NAE AFUATA NYAYO

ONANA AWAPAGAWISHA MASHABIKI MAPEMA SANA, NGOMA NAE AFUATA NYAYO

MABAO mawili ya Simba yaliyofungwa na Willy Onana na Fabrice Ngoma yametosha kufuta uteja kwa Simba kushindwa kupata matokeo mbele ya marais wa nchi wakishinda 2-0 dhidi ya Power Dynamos.

Onana ndiye alianza kuwapa furaha mashabiki wa Simba baada ya kufunga bao la kuongoza kipindi cha kwanza lililodumu hadi mapumziko huku bao la pili likifungwa kipindi cha pili.

Kipindi cha kwanza Simba walianza kwa kasi wakipasiana pasi fupi fupi na kuonana walionekana wakitumia winga za pembeni kutengeneza mashambulizi.

Mashambulizi yao yalikuwa yanasukwa na Willy Onana na Clatous Chama ambao walikuwa wanacheza kwa kubadilishana upande.

Onana alionekana kuwavutia zaidi mashabiki wa Simba kutokana na namna alivyokuwa anapiga pasi za uhakika kwa kufikisha kwa mtu sahihi.

Dakika ya 45 za kipindi cha kwanza zilithibitisha ufundi wake baada ya kukwamisha mpira nyavuni na kuwanyanyua mashabiki lukuki waliojitokeza kwa Mkapa.

Bao alilofunga lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika huku akimpa kicheko Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alipiga makofi baada ya mpira kukwama nyavuni.

Kipindi cha pili wapinzani wa Simba pamoja na kukosa bao la kufutia machozi walicheza kwa utulivu na kumiliki mpira tofauti na kipindi cha kwanza.

Simba wali fanya mabadiliko kwa kumtoa Willy Onana kaingia, Jean Balake, Clatous Chama katoka kaingia Luis Miquissone na ametoka Mzamiru Yassin kaingia Fabrice Ngoma, Hussein Kazi kaingia kuchukua nafasi ya Henock Inonga.

Pia akitoka Kibu Denis Alibhai Aubim Kramo, Saido Ntibazonkiza ameingia John Bocco pia wamemtoa Sadio Kanoute kaingia Abdallah Hamis.

SHABIKI AMVAMIA MIQUISSONE

Katika hali ya kushtusha shabiki ambaye hakutambulika haraka jina lake alitinga kiwanjani mpira ukiwa unaendelea na kumkumbatia kiungo Mshambuliaji wa timu hiyo Luis Miquissone.

Shabiki huyo aliluka kutoka jukwaa la viti vya rangi ya Machungwa na kuwazidi mbio walinzi hadi kumfikia Miquissone ambaye alibaki anatahamaki.

SOMA NA HII  AHMED ALLY AWAPIGA YANGA NA KITU KIZITO KIMYAKIMYA