Home Habari za michezo SALIM ALLY AISHIKA PABAYA SIMBA….. ISHU IKO HIVI

SALIM ALLY AISHIKA PABAYA SIMBA….. ISHU IKO HIVI

Habari za Simba SC

Bila kupepesa macho ukiambiwa utaje mchezaji bora wa michuano ya ngao ya jamii basi jina la Ally Salim utalikuta pale juu..to be honest kijana alikuwa na wakati mzuri sana, ukiachana na kupangua mikwaju ya penati bado alifanya Saves muhimu ndani ya dakika tisini ambazo ziliwapa ubingwa Simba.

Ni wazi sasa hivi kijana ana Confidence ya kutosha hivyo anahitaji kucheza mara kwa mara ili aendelee kupata uzoefu na ubora zaidi.

Lakini ukitazama orodha ya makipa wa Simba utagundua kuna Aishi Manula, Ayoub Lakred ambaye ni bingwa wa Morocco, Hussein Abel na Feruz.

Kusema Ukweli Manula na Ayoub Lakred wakiwa fiti ni ngumu Ally Salim kupata nafasi ya kucheza.

Hivyo kwa mtazamo wangu ili kulinda ubora wake Simba wanatakiwa kumtoa kwa mkopo kwenye timu ya daraja la kati mfano KMC au Mtibwa ili apate dakika nyingi za kutosha nadhani hilo litamuongezea vitu tofauti kwenye uchezaji wake pia atapata Confidence ya kutosha ili badae aje kuwa mrithi wa Manula.

Pia tukumbuke Ally Salim ndo kwanza ana miaka 22 hivyo kama golikipa bado ana uwanja mpana wa kufanya vizuri na kadri kipa anavyo kua ndivyo ubora wake unazidi kuongezeka.

Man United walipo hitaji ubora wa Dean Henderson walimtoa kwa mkopo vile vile Chelsea walipo hitaji ubora wa Thibaut Courtois, walimtoa kwa mkopo Atletico Madrid…..hivyo mkopo siyo dhambi.

SOMA NA HII  YANGA WAKOMAA NA PACHA WA NZEGELI.... ISHU IKO HIVI

2 COMMENTS

  1. “Amewashikaje” Simba pabaya? Title na body/content za habari yako hazioani. Uandishi wako wa hovyo. Mnakera!