Home Makala POKEA SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA SOKA LA BONGO…HUU NI ZAIDI YA...

POKEA SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA SOKA LA BONGO…HUU NI ZAIDI YA MWAKA KWAKO..UKO TAYARI..?


Habari Ndugu Msomaji, kwa kuzingatia umuhimu wako kwetu na kutambua mchango mkubwa unaoendelea kuutoa kwa kuwa mfuatiliaji wa habari na matukio yetu kwa mwaka uliopita, kwa niaba ya Uongozi wa Soka la Bongo , tunakutakia heri ya mwaka mpya .

Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kutuamini kwa mwaka jana na kuchagua kuwa upande wetu kwenye zaidi ya maelfu ya tovuti za michezo nchini, tunapenda kukufahamisha kuwa sisi bila wewe si kitu, na ndio maana kwa mwaka huu mpya tunakuhaidi kuendelea kukonga moyo wako kwa kukuletea habari motomoto zenye kusisimua na kufurahisha kuhusu michezo haswa kwa timu yako pendwa.

Ndani ya mwaka huu mpya, Soka la Bongo tunakuhaidi kuboresha huduma zetu , haswa kwa kuzingatia maoni ya maelfu ya wasomaji wetu, mathalani katika mwaka huu, tunatazamia kuja na kuitambulisha kwenu mitandao yetu ya kijamii, Instagram, Twitter na Youtube ili kuzidi kukusogeza karibu zaidi na matukio ya kimichezo nchini.

Pia katika kuongeza ufanisi, haswa kuzingatia maboresho tunayokusudia kuyafanya, tumepanga mwaka huu kutangaza nafasi za ajira kwa vijana na wote wenye vigezo vya kufanya kazi kwenye mitandao ya kijamii na tovuti, hivyo kuzidisha mchango wetu wa moja kwa moja kwenye jamii na taifa kwa ujumla.

Aidha , kwa mwaka huu pia tunatazamia kuanzisha tuzo za mashabiki, za SOKA LA BONGO FANS AWARDS ambazo kupitia kwazo, wewe msomaji wetu utashiriki kuchagua na kuzawadia tuzo kwa Klabu, Wachezaji ,vikundi na wadau wa michezo hususani mchezo wa Mpira wa Miguu Tanzania.

Hivyo kwa kuzingatia umuhimu wako kwetu, tunakuomba uyapokee mapendekezo haya ikiwa ni katika namna ya kuboresha na kufanya kitu cha tofauti ili kuzidi kuleta ladha tofauti katika tasnia ya habari na  mpira wa miguu nchini.

Yote kwa yote, tunakupenda sana na tunakutakia mwaka mpya wenye baraka, neema na fanaka tele kwenye maisha yako ya kila siku na MUNGU akutangulie kwenye kila jambo lenye kheri ulilopanga kulifanya kwa mwaka huu mpya.

SOMA NA HII  SENZO AVUNJA UKIMYA ISHU YA MABADILIKO YANGA...AFUNGUKA THAMANI HALISI YA YANGA..HAJI AJA NA HILI..

Happy New Year….

Mhariri Mtendaji

Soka la Bongo