Home news MUKOKO NDIO BASI TENA YANGA…ASHINDWA KUJIZUIA…AKUBALI YAISHE..AZAM YAMNYATIA…

MUKOKO NDIO BASI TENA YANGA…ASHINDWA KUJIZUIA…AKUBALI YAISHE..AZAM YAMNYATIA…


HUENDA kiungo mkabaji wa Yanga, Mkongomani, Mukoko Tonombe akatua kwa mkopo Azam FC katika usajili huu wa dirisha dogo.

Usajili huo ulifunguliwa Desemba 16, mwaka huu na Yanga tayari imemtambulisha kiungo Salum Abubakari ‘Sure Boy’ aliyeomba kuondoka Azam FC.

Mukoko anatajwa huenda akatimka Yanga kwa kile kinachotajwa hana furaha ya kuendelea kukipiga hapo baada ya kukosa nafasi ya kucheza msimu huu.

Taarifa ambazo zimepatikana, zinasema kwamba, Mukoko kwa kupitia menejimenti yake inayomsimamia, imeomba kiungo huyo aondoke kwa mkopo.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa Azam ndiyo timu ya kwanza kupeleka maombi ya kumtaka Mukoko kwa mkopo wa miezi sita aliyoibakisha katika mkataba wake ndani ya Yanga.

“Katika kuhakikisha analinda kipaji chake, uongozi wa Yanga huenda ukamtoa kwa mkopo Mukoko baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

“Hiyo ni baada ya menejimenti ya Mukoko kupendekeza mchezaji wao aondoke kwa mkopo na timu inayopewa nafasi kubwa ni Azam ambayo yenyewe imeonesha nia ya kumuhitaji.

“Kama mazungumzo yatakwenda vizuri, basi Mukoko atakwenda kwa mkopo Azam katika usajili huu wa dirisha dogo,” alisema mtoa taarifa huyo.

SOMA NA HII  TATIZO WABONGO TUNADHARAU SOKA LETU...SIMBA NA YANGA NI TISHIO KUBWA CAF