Home Uncategorized MTAMBO WA MABAO WAWAAMBIA YANGA IWEKE MKWANJA ASAINI

MTAMBO WA MABAO WAWAAMBIA YANGA IWEKE MKWANJA ASAINI


NYOTA wa kikosi cha JKT Tanzania, Adam Adam amesema kuwa ikiwa mabosi wa Yanga wataweka mkwanja unaoeleweka atamwaga wino bila mashaka.

Adam mwenye mabao saba ndani ya Ligi Kuu Bara imekuwa ikitajwa kuwa anahitajika na mabosi wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

Akizungumza na Saleh Jembe, Adam amesema kuwa ikiwa Yanga watakuwa wanahitaji saini yake ni suala la kuweka mkwanja mezani na akiona unamstahili atamwaga wino.

“Mimi ni mchezaji na uwezo wangu upo wazi ikiwa Yanga watakuwa wanahitaji saini yangu ni suala la kuzungumza na uongozi wangu na dau likiwa kubwa mimi nitasaini.

“Ipo wazi kwamba kwa sasa kuna timu ambazo zinahitaji saini yangu ila kwa kuwa bado mambo hayajawa rasmi ikiwa wazi nitaweka wazi,” .

SOMA NA HII  REAL MADRID KUUZA NYOTA WATANO KUMPATA NYOTA WA MANCHESTER UNITED