Home Uncategorized REAL MADRID KUUZA NYOTA WATANO KUMPATA NYOTA WA MANCHESTER UNITED

REAL MADRID KUUZA NYOTA WATANO KUMPATA NYOTA WA MANCHESTER UNITED

REAL Madrid ipo kwenye mpango wa kuwauza nyota wake watano ili kupata pauni milioni 200 kwa ajili ya kumnunua kiungo wa Manchesster United, Paul Pogba.
Nyota huyo raia wa Ufaransa anahusishwa kujiunga na Real Madrid ambao wapo kwenye hekaheka za kuipata saini yake.
Inaelezwa kuwa Madrid inatazamia kuwauza Gareth Bale, James Rodriguez, Dani Ceballos, Marco Asensio na Isco ili kukusanya mkwanja huo.
Atletico Madrid na Napoli zinahitaji kumpata Rodriguez huku Arsenal na Tottenham zikiwania saini ya Ceballos.
Asensio na Isco bado wanatazamwa kama wanaweza kuingia kwenye mipango ya Real Madrid ila haijawa wazi kama meneja, Zinedine Zidane ana mpango nao msimu ujao.
SOMA NA HII  FAINALI YA CECAFA LEO,UGANDA V NGORONGORO