Home Uncategorized LEICESTER CITY YAZIKAZIA MANCHESTER CITY NA UNITED KWA BEKI WAO

LEICESTER CITY YAZIKAZIA MANCHESTER CITY NA UNITED KWA BEKI WAO


BRENDAN Rodgers bosi wa Leicester City amethibitisha kwamba tayari timu yake imeachana na ofa za timu mbili ambazo zilikuwa zinahitaji huduma ya beki wao wa kati Harry Maguire.

Licha ya ofa hizo mbili kwa nyota huyo wa Taifa la England ambaye alikuwa sehemu ya kikosi kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Scunthorpe siku ya Jumanne na waliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Maguire amezivutia timu nyingi kubwa ikiwa ni pamoja na Manchester United na Manchester City ambao walikuwa wanahitaji huduma yake kwa dau la thamani ya pauni milioni 90.
“Harry ni mchezaji wa thamani ya juu na ana uwezo mkubwa inakuwa ni ngumu kwa sasa timu kukubali kumuuza, zipo timu ambazo zinamhitaji ila bado tunaona ni kijana mzuri kwetu na ana uhakika wa kupata namba kama ambavyo alifanya kwenye dakika 45 alizocheza,” amesema.

SOMA NA HII  JAGUAR AFIKISHWA MAHAKAMANI, ATAENDELEA KUSOTA RUMANDE KAMA KAWA