Home Uncategorized HUYU NDIYE ALIYE NYUMA YA USAJILI WA NYOTA WA SIMBA FRANCIS KAHATA

HUYU NDIYE ALIYE NYUMA YA USAJILI WA NYOTA WA SIMBA FRANCIS KAHATA


FRANCIS Kahata kiungo mpya wa Simba amesema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wamechangia kumshawishi ajiunge ndani ya kikosi hicho ni mshambuliaji Meddie Kagere.

Kahata amejifunga kwa kandarasi ya miaka miwili ndani ya Simba akitokea timu ya Gor Mahia ambayo Kagere naye aliwahi kuitumikia.

“Nilikuwa nina ofa nyingi mbali na Simba kutokana na ukubwa wa klabu na ukaribu wangu na Kagere sikuona haja ya kwenda mbali nikakubali kujiunga na Simba.

“Kwa sasa ninafuraha kwa kuwa nimeona timu ipo vizuri na ina mipango mingi mizuri hivyo kwa kushirikiana nao nina amini tutafanya vema,” amesema Kahata.

SOMA NA HII  YANGA NA PACOME MPAKA AFCON