Home Uncategorized SIMBA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA RUVU SHOOTING

SIMBA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA RUVU SHOOTING


 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba leo ana kibarua cha kumenyana na Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni.


Sven ambaye inaelezwa kuwa anavuta dola 9,000 ambazo ni sawa na Sh 20.7Mil kwa mwezi ataingia uwanjani akiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Tanzania Prisons.


Ruvu Shooting imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Uhuru.


Raia huyo wa Ubelgiji amesema kuwa anaamini mchezo wa leo utakuwa na ushindani mkubwa ila wanahitaji pointi tatu muhimu.


“Ni mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa, imani yangu ni kwamba wachezaji wanajua kwamba mchezo uliopita tumepoteza, ila tutafanya vizuri kwenye mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting.


“Mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu yao na tuna amini kwamba tutafanya vizuri,” amesema.


Msimu uliopita walipokutana Uwanja wa Mkapa mchezo wa mwisho, Simba ilikubali sare ya kufungana bao 1-1 hivyo leo kazi itakuwa kubwa kwa timu hizi mbili.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA AIPA TAHADHARI YANGA KWA ZESCO