Home Uncategorized AZAM FC KUWAKOSA NYOTA WAWILI LEO WAKIIVAA MTIBWA SUGAR

AZAM FC KUWAKOSA NYOTA WAWILI LEO WAKIIVAA MTIBWA SUGAR


LEO Azam FC inashuka Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kumenyana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.


Azam FC ikiwa imecheza mechi saba imefikisha pointi 21 kibindoni inakutana na Mtibwa Sugar ambayo imecheza mechi saba na pointi zake nane.


Kwenye mchezo wa leo Azam FC itawakosa nyota wake wawili ambao wamehusika kwenye mabao saba kati ya 14 ambayo yamefungwa na timu hiyo inayonolewa na Aristica Cioaba.


Obrey Chirwa mwenye mabao manne na pasi mbili za mabao anasumbuliwa na enka huku kiungo Salum Abubakar, ‘Sure Boy’ mwenye pasi moja ya bao yeye ana kadi tatu za njano.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wana imani ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo licha ya kuwakosa nyota wawili kikosi cha kwanza.


“Tutawakosa wachezaji wawili ambao ni Chirwa,(Obrey) na Sure Boy licha ya kwamba hawatakuwepo bado tumejipanga kupata ushindi kwenye mchezo wa leo,” amesema.

SOMA NA HII  KOCHA KAGERA SUGAR AWATAKA WACHEZAJI WASIPUUZIE MAZOEZI