Home Uncategorized KAZE: KAZI BADO IPO, WACHEZAJI WANA UWEZO MKUBWA

KAZE: KAZI BADO IPO, WACHEZAJI WANA UWEZO MKUBWA


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anafurahishwa na uwezo wa nyota wake wote ndani ya kikosi hicho jambo ambalo anaamini litakuwa nguzo kubwa kufikia malengo.


Jana Oktoba 25, Kaze alikiongoza kikosi chake kwenye mchezo wa pili mbele ya KMC Uwanja wa CCM Kirumba na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.


Nyota wa mchezo wa jana alikuwa ni Wazir Junior ambaye alifunga bao la ushindi kwa Yanga akitumia pasi ya nyota mwenzake Farid Mussa.


Kaze amesema:”Ni jambo jema kuona kwamba kila mchezaji ni muhimu kikosi cha kwanza anafanya vile ambavyo nimemuagiza.


“Uzuri ni kwamba kila mchezaji ni muhimu na anatambua majukumu yake akiwa ndani ya uwanja ni mwanzo mzuri utatupa mwanga kufika kule ambako tunafikiria.

“Taratibu kila mchezaji anaimarika na kuwa imara ndani ya kikosi ninapenda kuona namna ambavyo wachezaji wanajituma pamoja na sapoti kutoka kwa mashabiki hivyo bado kuna kazi ya kufanya,” amesema.


Mchezo wa kwanza Kaze kukaa benchi alishinda bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Uhuru na jana ameshinda  mchezo wake wa pili mbele ya KMC Uwanja wa CC Kirumba.


Yanga inafikisha jumla ya pointi 19 ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi saba ndani ya Ligi Kuu Bara na kinara ni Azam FC mwenye pointi 21 akiwa amecheza mechi saba. 

SOMA NA HII  BEKI SIMBA AKUBALI UWEZO WA SAIDO WA YANGA