Home Habari za michezo KISA KELELE ZA ‘SUB’ YA CHAMA…MBRAZILI SIMBA KAWASIKIA…KISHA AKAJIBU HIVI KIBABE YANI…

KISA KELELE ZA ‘SUB’ YA CHAMA…MBRAZILI SIMBA KAWASIKIA…KISHA AKAJIBU HIVI KIBABE YANI…

Habari za Simba

Huku kukiwa na maoni tofauti baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City, Kocha Mkuu wa Simba , Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema kwa sasa anahitaji kupata ushindi bila kujali wachezaji wake wanachezaje kutokana na ushindani uliopo katika mbio za kuwania ubingwa

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Robertinho, Saido Ntibazonkiza akifunga magoli mawili na lingine likipachikwa wavuni na Pape Osman Sakho.

Robertinho, alisema jambo lake la kwanza alikuwa anahitaji kuvuna pointi tatu muhimu, jambo ambalo alifanikiwa na limemfanya afurahie ushindi huo wa mechi yake ya kwanza.

Robertinho alisema amefurahishwa na namna wachezaji walivyocheza kwa ushirikiano licha ya kukaa nao kwa muda mfupi, wameonyesha kile alichowaelekeza katika siku chache alizokaa nao.

“Nilihitaji ushindi bila kujali tumechezaje, tupo katika mbio za ubingwa, tunapaswa kushinda kila mchezo hasa tunapokuwa nyumbani, ndio kwanza nina siku nane tangu nilipoanza kazi, Simba ni timu kubwa na malengo yake ni makubwa kama nilivyo mimi.

Jambo jingine lililonifurahisha ni jinsi tulivyocheza, wachezaji walicheza kitimu ingawa kulikuwa na makosa kadhaa ambayo tunapaswa kuyaondoa, nimeanza kupata mwanga wa kikosi ambacho kinapaswa kiwe, ninaimani mechi zijazo watacheza vizuri zaidi ya mechi ya leo (juzi),” alisema Robertinho.

Kocha huyo alisema kuhusu mabadiliko aliyoyafanya ni baada ya mchezaji wake kupata majeraha na kuogopa kuendelea kumtumia kwa sababu ya kuhofia kumuumiza na kupata jeraha kubwa zaidi na kufanya kukaa nje kwa muda mrefu.

Kuhusu kiungo, Clatous Chama, alisema aliondolewa baada ya kupata maumivu ya mguu na kuhitaji kufanyiwa mabadiliko kwa sababu hakuwa na uwezo wa kuendelea kuipambania timu.

“Nashukuru Mungu nilifanikiwa kutoa pasi na kupata bao la kwanza, nilisikia maumivu mguuni na sikuweza kuendelea kucheza na kuonyesha kiwango kizuri na kocha (Robertinho) aliona hilo na kufanya mabadiliko kwa ajili ya kufikia malengo yetu ya kutafuta pointi tatu jambo ambalo tumefanikiwa,” alisema Chama.

Naye Kocha Mkuu wa Mbeya City, Abdallah Mubiru, alisema wachezaji wake wamepambana lakini bahati haikuwa upande wao kwa kuruhusu kupoteza mchezo huo jambo ambalo halikuwa katika malengo yao.

Mubiru alisema malengo makubwa katika mchezo huo yalikuwa kutafufa pointi tatu au kuondoka na alama moja licha ya kuamini wao ndio walitawala mpira kwa asilimia kubwa dhidi ya Simba.

“Niwapongeze wachezaji wangu kwa kuonyesha mchezo mzuri dhidi ya Simba iliyopata ushindi baada ya kutumia mapungufu yetu, tunaenda kujiandaa na mchezo ujao,” alisema Mubiru.

Simba iko Dodoma kuwafuata wenyeji Dodoma Jiji FC katika mechi nyingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa kesho na baada ya hapo itarejea Dar es Salaam kuwasubiri Coastal Union kwenye mchezo wa hatua ya 32 Bora ya mashindano ya Kombe la FA.

Wekundu wa Msimbazi ndio wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia kwenye mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati watani zao Yanga wao watachuana katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, timu zote zimetinga hatua ya makundi.

SOMA NA HII  HII HAPA SABABU YA GEORGE MPOLE KUBAKI SEBULENI CONGO WAKATI TIMU YAKE IKICHEZA....