Home Uncategorized MRITHI WA FRAGA NDANI YA SIMBA KUANZA KUONYESHA MAKEKE YAKE, WENGINE WANAKUJA

MRITHI WA FRAGA NDANI YA SIMBA KUANZA KUONYESHA MAKEKE YAKE, WENGINE WANAKUJA


KIUNGO mpya wa Simba, Taddeo Lwanga ataanza kuonyesha makeke yake ndani ya uwanja baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa.


Dirisha la usajili linatarajiwa kufunguliwa Desemba 15 ambapo tayari Simba imeshakamilisha usajili wa kiungo huyo mkabaji raia wa Uganda kwa dili la miaka miwili kutumika ndani ya klabu hiyo.


Anakuwa mrithi wa Gerson Fraga raia wa Brazil ambaye amechimbishwa ndani ya Simba jumlajumla kutokana na kuwa na majeraha ya muda mrefu na ameshafanyiwa upasuaji wa goti ila yupo zake nchini Brazili.

Lengo kubwa la Simba kumvuta nyota huyo ni kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo mkabaji ambapo atakuwa akishirikiana na mzawa Jonas Mkude, Mzamiru Yassini pamoja na Said Ndemla.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mpango kazi mkubwa ni kuendelea kufanya zoezi hilo la usajili kuwa endelevu na watashusha wachezaji wengine.

“Zoezi la usajili tutakaowasijili litakuwa endelevu na huyu Lwanga ni chuma kipya hivyo wengine wanakuja,” amesema. 

SOMA NA HII  HII HAPA RATIBA YA MECHI ZA YANGA