Home Uncategorized KMC YAWAITA MASHABIKI KUSHUHUDIA PIRA SPANA KESHO UHURU

KMC YAWAITA MASHABIKI KUSHUHUDIA PIRA SPANA KESHO UHURU

 


WAKATI Simba wakitamba kwa mashabiki wao na pira biriani ndani ya uwanja, Coastal Union pira nazi, Azam FC pira Ice Cream, KMC imewaambia mashabiki kuwa wajitokeze kesho kuona ‘piraspana’ dhidi ya Dodoma Jiji.

KMC ikiwa nafasi ya 8 na pointi 18 baada ya kucheza mechi 11 inakutana na Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 9 na pointi 16 ikiwa imecheza mechi 12.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wachezaji wamepewa mbinu nyingi na makocha wao wawili ambao ni wazawa jambo linalowapa matumaini ya kupata pointi tatu.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Uhuru kushuhudia pira spana kutoka kwa KMC, mbinu za John Mkoko ambaye ni Kocha Mkuu na Habibu Kondo zitaonekana ndani ya uwanja,” amesema Christina.

Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa KMC kuikaribisha Dodoma Jiji kwa kuwa imepanda daraja msimu huu wa 2020/21.

 

 

SOMA NA HII  SIMBA LEO KUKIPIGA DHIDI YA KMC NA TRANSIT CAMP, MUGALO KUZIKOSA ZOTE MBILI