Home Uncategorized KOCHA STARS: TEKNOLOJIA MPYA ITANIRAHISISHIA KAZI

KOCHA STARS: TEKNOLOJIA MPYA ITANIRAHISISHIA KAZI


KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije amesema kuwa teknolojia mpya inayotumika ndani ya timu hiyo kwa sasa itamrahisishia kazi ya kutambua muda na uwezo wa wachezaji wake wakiwa  kwenye mazoezi.

Ndayiragije amesema kuwa kwa sasa wachezaji wanatumia vifaa maalumu ambavyo wanavivaa (GPS) wakiwa mazoezini vitasaidia kutambua utimamu wa mwili kwa wachezaji.

“Vifaa wanavyovaa wachezaji wakiwa mazoezini vinasaidia kutambua utimamu wa mwili pamoja na uwezo wao na muda ambao wamefanya mazoezi hiyo inarahissha katika kutambua ubora wao.

“Hivi pia vimekuwa vikitumiwa na wachezaji wakubwa katika kufanya kwao mazoezi ni kitu kizuri na nina imani kitakuwa na matokeo chanya,” amesema.

SOMA NA HII  NDONDO CUP KUMENOGA, BAKHRESA YAONGEZA NGUVU