Home Uncategorized YANGA YAANIKA MIPANGO ITAKAYOTUMIA KUIMALIZA SIMBA MACHI 8

YANGA YAANIKA MIPANGO ITAKAYOTUMIA KUIMALIZA SIMBA MACHI 8


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa, mechi nne zijazo ambazo ni sawa na dakika 360, watazitumia kwa ajili ya maandalizi ya kuiangamiza Simba

Yanga ambayo jana Jumamosi ilipambana na Prisons kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, itapambana na Simba Machi 8, mwaka huu uwanjani hapo.

Kabla ya kupambana na Simba, itakuwa na kibarua cha kucheza mechi nne dhidi ya Polisi Tanzania, Coastal Union, Alliance na Mbao. Katika mechi hizo, mbili dhidi ya Polisi na Coastal ndizo watachezea ugenini. Zilizobaki nyumbani.

“Tuna mechi nyingi kabla ya kukutana na Simba na zote hizo ni ngumu, hivyo lazima tupambane kwa mpangilio mzuri, mechi hizo zitatupa hali ya kujiamini na kutengeneza kikosi maalumu kitakachotupa nguvu ya kuiangamiza Simba.

“Nafahamu kwamba huwezi kutengeneza kikosi bora iwapo utashindwa kuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo, kwa sasa nataka wachezaji wangu wacheze vizuri kabla ya mchezo huo na huwa ninawaambia kwamba silali kwa ajili ya kuwaza mbinu mpya za kushinda mechi zetu,” alisema Luc.

MIPANGO YA KUISHUSHA SIMBA

Katika hatua nyingine, kocha huyo amesema kuwa njia ya kuishusha Simba kutoka nafasi ya kwanza iliyopo sasa ni wao kushinda mechi zao zote zilizobaki.

Kabla ya mechi za jana Jumamosi, Yanga ilikuwa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 38 ikicheza mechi 19 na Simba ikiongoza ligi ikijikusanyia pointi 53 katika mechi 21. Tofauti yao ni pointi 15.

Baada ya mechi za jana, Simba imebakiwa na mechi 16 ambazo ni sawa na pointi 48, huku Yanga mechi zao 18 zilizobaki ni sawa na pointi 54.

Akizungumza na Spoti Xtra, Luc alisema kuwa ana mlima mkubwa wa pointi anazodaiwa na Simba jambo ambalo linamfanya apasue kichwa kufikiria namna ya kumalizana nao.

“Simba ni wapinzani wetu wakubwa ambao kwa sasa wapo nafasi ya kwanza, nimewaambia wachezaji wangu kwamba jambo moja tu litakalowashusha wapinzani wetu pale walipo ni sisi kushinda mechi zetu zote.

“Kushinda mechi zote zilizobaki inawezekana endapo wachezaji watafuata maelekezo ninayowapatia,” alisema kocha huyo.

Kauli ya kocha huyo iliungwa mkono na viungo wake, Papy Tshishimbi na Haruna Niyonzima ambao wameapa watashinda kila mchezo ulio mbele yao hadi mwisho wa ligi.

Niyonzima alisema: “Kwa sasa tunaangalia mbele kwa mbele, hatuna sababu ya kurudi nyuma, kule tulikotoka hatukuwa katika hali nzuri, ila kwa sasa timu ipo vizuri, wachezaji wote tuna morali ya juu. Kila mchezo tutacheza kama fainali ili tushinde yote.”

Naye Tshishimbi alisema: “Si rahisi kupata pointi tatu katika kila mchezo, lakini sisi tutapambana kuhakikisha tunatimiza malengo kwa kushinda mechi
SOMA NA HII  JUMA MGUNDA AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE