Home Uncategorized NDONDO CUP KUMENOGA, BAKHRESA YAONGEZA NGUVU

NDONDO CUP KUMENOGA, BAKHRESA YAONGEZA NGUVU


MICHUANO ya Ndondo Cup msimu wa mwaka 2019 imezidi kunoga baada ya kampuni ya vinywaji ya Bakhresa tawi la Magomeni Icecream kuongeza nguvu ya udhamini kwenye michuano hiyo ambayo imejipatia umaarufu kwa sasa ikiwa na lengo la kuinua na kukuza vipaji itaanza Juni 17 mwaka huu.

Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari leo, Mwenyekiti wa Ndondo Cup, Shafii Dauda amesema kuwa malengo makubwa ni kuona mashindano yanakuwa bora  na kila mmoja anayekwenda kushuhudia michuano hiyo anapata kilicho bora zaidi.

“Kwa kuanza  kila shabiki atakayeingia uwanjani atapewa kinywaji cha bure baada ya kununua tiketi kuangalia michuano ya Ndondo kama atahitaji kinywaji kingine atapata kwa bei maalumu ambayo ni punguzo kwa wale watakaokuwepo uwanjani,” amesema.

Msimamizi wa kituo cha Magomeni Ice cream, Ibrahim Wasome, amesema, vinywaji vyote vya Bakhresa Food Products vitauzwa kwa bei maalum ndani ya viwanja vya Ndondo Cup ukilinganisha na bei ya mtaani.

“Msimu huu wa mashindano ya Ndondo Cup utakuwa wa kipekee na utavutia, vinywaji vya Bakhresa vitauzwa kwa bei maalum ya Ndondo Cup, kwa kila chupa kutakuwa na kuponi maalumu .

“Mfano maji ya Uhai ya Sh.700 yatauzwa Sh. 600, maji ya Shilingi 300 yatauzwa Sh. 200. Kwa kifupi kutakuwa na punguzo la shilingi 100 kwa kila kinywaji, ni kifurushi maalumu cha Ndondo, mashabiki wajitokeze kwa wingi kupata burudani,” amesema.

SOMA NA HII  HIZI HAPA MECHI 19 ZA YANGA MZUNGUKO WA KWANZA 2019-20