Home Uncategorized BAADA YA ZALI KUWAANGUKIA YANGA NA KMC SIMBA WATOA TAMKO

BAADA YA ZALI KUWAANGUKIA YANGA NA KMC SIMBA WATOA TAMKO

BAADA ya Shirikisho la Soka Afrika kuthibitisha kwamba rasmi Tanzania itashirikisha timu nne michuano ya kimataifa kutokana na kukidhi vigezo hasa baada ya kushika nafasi ya 12 kwa ubora, uongozi wa Simba umetoa tamko kwa timu zitakazoshiriki.

Kuongezeka kwa timu moja kila michuano inafanya Tanzania kufikisha jumla ya timu nne ambazo kwa upande wa Ligi ya Mabingwa ni Simba na Yanga huku kwa upande wa kombe la Shirikisho ni Azam FC na KMC.

Mafanikio ya soka kwa Tanzania yamechangiwa na mabingwa hao ambao msimu uliopita walifika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika hali iliyofanya nafasi ya Tanzania kupanda kwa ubora mpaka nafasi ya 12.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ni zamu ya timu zilizopta nafasi ya kushiriki kimataifa kupeperusha vema Bendera ya Tanzania.

” Nafasi hii adimu ambayo imeipata nchi yetu ya Tanzania ni kwa mara ya kwanza tunapeleka timu nne katika mashindano ya Caf, hivyo kwa waliopata nafasi ni muda wa kufanya kweli na sio kuturudisha tulikotoka,” amesema Manara.


SOMA NA HII  MBEYA CITY V SIMBA NGOMA NZITO LEO SOKOINE