Home Uncategorized KIUNGO WA YANGA KUIBUKIA AFRIKA KUSINI

KIUNGO WA YANGA KUIBUKIA AFRIKA KUSINI

 


NYOTA wa kikosi cha Yanga kiungo Mapinduzi Balama muda wowote kuanzia sasa anaweza kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.


Balama alipata maumivu ya mguu wa kushoto msimu uliopita wakati timu yake ikiwa kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC.


Kwa sasa ameendelea kupewa huduma ya matibabu huku akishuhudia wenzake wakiendelea kupambana kupata matokeo ndani ya uwanja.


Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija amesema kuwa kiungo huyo atakwenda Afrika Kusini ili kufanyiwa uchunguzi zaidi baada ya kukosekana uwanjani kwa muda mrefu.


“Ni kweli Balama Mapinduzi anaelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa zaidi vipimo vya afya yake ili kuendelea mchakato na maendeleo yake.


“Taarifa zake tutaendelea kuzitoa kwani kwa sasa bado hatujajua kwamba itamchukua muda gani huko,” amesema.


Mapinduzi atakumbukwa kwa uwezo wake wa mashuti akiwa nje ya 18 ambapo aliibuka shujaa kwenye dabi dhidi ya Simba alipomtungua Aishi Manula na kufanya Simba isiamini ilichokiona kwani baada ya dakika 90 ngoma ilikuwa 2-2.

SOMA NA HII  MBEYA CITY YAINGIA LEVEL ZA JUVENTUS NA LEICESTER CITY