Home Habari za michezo HAJI MANARA AUMBUKA…NI BAADA YA KUMGOMBANISHA RAISI YANGA NA MTANGAZAJI

HAJI MANARA AUMBUKA…NI BAADA YA KUMGOMBANISHA RAISI YANGA NA MTANGAZAJI

HAJI MANARA AUMBUKA...NI BAADA YA KUMGOMBANISHA RAISI YANGA NA MTANGAZAJI

Taarifa zisizothibitishwa zimeenea mitandaoni kuhusu Mchambuzi wa masuala ya michezo nchini kutoka Kituo cha televisheni cha Channel Ten, Juma Ayo kuwa alimuomba pesa Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said ili akamtibie ndugu yake.

Taarifa hizo zilizochapishwa na na Msemaji wa Yanga, Haji Manara zinaeleza kuwa Hersi alimnyima pesa kijana huyo ndio maana yeye na wachambuzi wenzake wana chuki na Yanga na kufanya wazue taarifa za uongo kuhusu Yanga mara kwa mara.

Juma Ayo ameibuka na kujibu shutuma hizo akisema; “Kwa heshima ya klabu ya Yanga na viongozi wake niseme tu hakuna mazungumzo yangu na Engineer kumuomba pesa.

“Nitaendelea kutunza mazungumzo mbalimbali nayofanya na viongozi wa mpira kwa lengo la kudumisha amani na uadilifu.

“Tujikite kwenye football tuachane na personalities. Tuendelee kuzungumzia mpira na si mambo binafsi ya watu,” amesema Juma Ayo.

SOMA NA HII  KAULI HII YA SOPU KWA AZAM FC NI KAMA MASTAA ULAYA WANAVYOFANYAGA WAKISAJILIWA TIMU MPYA...