Home Habari za michezo KOCHA SIMBA SC AWAPUUZA WYDAD CA…”NAWAJUA HAWASUMBUI…AMEZUNGUMZA HAYA

KOCHA SIMBA SC AWAPUUZA WYDAD CA…”NAWAJUA HAWASUMBUI…AMEZUNGUMZA HAYA

Habari za Simba SC

Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazil Robert Oliveira ‘Robertinho’ amefunguka kuwa licha ya kuwajua wapinzani wake katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini amewataka wachezaji kuacha kuwafikiria Wydad Casablanca kwa kuwa bado wana mchezo mgumu dhidi ya Yanga.

Robertinho ametoa kauli hiyo ikiwa Simba kwa sasa inakabiliwa na mchezo mmoja ya Ligi Kuu Bara kabla ya kucheza mchezo wa kwanza robo fainali dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco katika mchezo unaotarajia kupigwa Aprili 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Kabla ya mchezo huo Simba itawavaa Yanga katika mchezo utakaopigwa Aprili 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza nasi, Robertinho alisema kuwa wachezaji wake kwa sasa hawapaswi kuweka nguvu kubwa ya presha katika mchezo wao robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwa bado wana mechi ngumu za ligi Kuu ikiwemo dhidi ya Yanga.

“Kitu ambacho tulikuwa tunakisubiria ni kujua tutakutana na timu gani katika hatua ya robo fainali lakini siyo kuweka nguvu kubwa huko tukiwa bado tuna mechi nyingine ngumu katika Ligi Kuu Bara, tunatakiwa kucheza na Yanga ambapo tunataka matokeo.

“Kila mchezaji anatambua kuwa malengo yetu yapo kutoka mechi moja kwenda katika mechi nyingine kwa sababu tumeshajua nani tutacheza naye lazima tuweke nguvu kubwa kwenye hizi mechi za ndani kwa sababu ukiangalia mchezo dhidi ya Yanga ambao wanaongoza ligi hautokuwa wa kawaida kutokana upinzani wa jadi uliopo kati yetu,” alisema Robertinho.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUTOLEWA KWA MBINDE JANA...RAIS SAMIA ATOA AHADI HII KWA YANGA...