Home Habari za michezo SAKATA LA YANGA KUTOALIKWA MKUTANO WA CAF ….TFF WAIBUKA NA MAJIBU HAYA...

SAKATA LA YANGA KUTOALIKWA MKUTANO WA CAF ….TFF WAIBUKA NA MAJIBU HAYA YA ‘KIBABE’…WAJIVUA KOTI MAPEMA TUU…


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba wadau kupuuza taarifa potofu zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuhusu mialiko ya Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) uliofanyika jana nchini Tanzania.

Mkutano huo wa 44 wa CAF uliofanyika jijini Arusha uliandaliwa na Shirikisho hilo, na TFF ilikuwa mwenyeji.

Wajumbe wa Mkutano huo wametajwa katika Katiba ya CAF, na waalikwa wengine nao wanaalikwa na Shirikisho hilo na si TFF kama inavyopotoshwa.

Nafasi ya TFF ilikuwa ni kutafuta mgeni rasmi wa kufungua Mkutano huo, si vinginevyo.

Ukiondoa Kamati ya Ndani ya Maandalizi (LOC), washiriki wengine wote walialikwa na CAF yenyewe.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUIFUNGA TZ 3-0....KOCHA WA MOROCCO AFUNGUKA ALICHOKIONA KWA STARS....